Header Ads 728*90

TAMMY, AFUNGUKA CHANGAMOTO KWENYE MUZIKI


                                                                              
MUZIKI wa hip hop unazidi kukua nchini japo idadi ya wasanii wa kike bado ni ndogo kwenye tansia ya muziki huo, Tamara Ally(Tammy The Baddest) jana amefunguka kuhusiana na matatizo na changamoto alizokutana nazo katika muziki.

Akizungumza katika mahojiano na televisheni moja hapa nchini, alisema kuwa moja ya changamoto aliyokutana nayo alipoanza muziki, ni wazazi wake kutokubaliana na swala la yeye kufanya muziki, hali iliyompelekea kuchelewa kuingia kwenye game ya muziki.
“Wazazi wangu walikuwa hawataki mimi nijishughulishe na maswala ya muziki, kwa sababu nilikuwa nasoma bado na baba yangu kipindi hicho alikuwa muathirika na madawa ya kulevya, kutokana na hilo alishindwa kutimiza majukumu yake kama mzazi, jambo hilo lilileta ugumu wa mimi kuingia kwenye muziki”. Tammy alisema.

Jamii kwa ujumla nayo imekuwa na mtazamo hasi, hasa kwa watoto wa kike ambao wanajitosa kutafuta liziki kupitia muziki wa hip hop, na kuona kuwa muziki huo sio utamaduni wa kiafrika kwani unamuondolea heshima mtoto wa kike kwenye jamii na kutothaminika.
Aliendelea kusema ilifika kipindi wasanii wa kiume wanaofanya miziki wa hip hop na anao waheshimu wanapokuwa kwenye mahojiano na vituo mbalimbali vya habari wakimponda kwa kusema anamuiga Nick Minaj na pia hajui kurap, hali hiyo ilimvunja moyo na kumfanya achelewe kuingia kwenye kiwanda cha burudani.
Kwa sasa TammytheBaddest anatamba na kibao chake kipya cha Mtoto wa Kike ambacho jumapili iliyopita aliachia video ya nyimbo hiyo na sasa inafanya vizuri katika televisheni tofaut tofauti hapa nchini.

No comments

Powered by Blogger.