TRUMP KUITEMBELEA UINGEREZA MWAKANI
Rais wa Marekania
Donald Trump anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza mwaka ujao.
Bwana Trump alikubali
mwaliko wa Malkia wa kumuomba afanye ziara nchini Uingereza wakati waziri mkuu
Theresa May alifanya ziara nchini Marekani mwezi Januari.
Lakini ziara hiyo
ilizua utata na hadi hata kusababisha Trump kubadili fikra zake.
Inaripotiwa kuwa
hakutaka kuifanya ziara hiyo wakati kuna upinzani dhidi yake.
Mwezi Mei karibu watu
milioni mbili walisaini ombi la kusema kuwa Trump haruhusiwa kuingia nchini
Uingereza.
Wanasiasa wakuu
akiwemo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn, na aliyekuwa kiongozi wa
chama cha Lib Dem Tim Farron walitaka ziara hiyo kufutwa.
Maswali yaliibuka
kuhusu ni kwa nini Trump alialikwa muda mfupi baada ya kuingia ofisini.
No comments