BARCA YAPOOZA MAUMIVU YA JUVE KWA MADRID
Na John Richard
BAADA ya mabingwa mara tano wa Uefa champion leage,
Barcelona kuondoshwa na vibibi kizee vya Torino katika hatua ya robo fainali,
wamehamishia hasira zao kunako Laliga kuusaka uchampioni huo kwa ali na mali.
Barcelona iliingia uwanjani ikiwa nyuma point 3
mbele ya mahasimu wao Real Madrid ambao wana faida ya mchezo mmoja mkononi na bado
wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano ya Uefa Championi
Leage hali inayo wafanya kuwania makombe mawili msimu huu.
Madrid walikuwa wanahitaji ushindi katika mchezo wa
jana ili kujihakikishia nafasi ya kutwaaa ubingwa wa Ligi kuu ya Hispania
alimaarufu kama Laliga walioukosa kwa takribani misimu mine iliyopita.
Alikuwa Casimiro
aliyeiandikia Madrid bao la kwanza kunako dakika ya na Lion Mess kuisawazishia Barcelona kunako
dakika ya hadi mapumziko Real Madrid 1 Barcelona 1. Licha ya mchezo huo kuwa
wavuta nikuvute kwa pande zote mbili.
Kunako kipindi cha pili timu zote zililejea huku
kila timu ikionekana kuwa na mipango mingi ya kutafuta mabao, Latcht alikuwa
shujaa kwa kuwainua mashabiki wa Barcelona kwenye viti vya Santiago Bernabeu kwa
mara ya pili.
James Rodriquez super sub, anaisawazishia Madrid bao
la pili kunako dakika ya 86, aliyeingia baada ya Madrid kupata pigo la kutolewa
kwa Sergio Ramos kwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo kwa kudhani kuwa
amemchezea Lion Mess lafu.
Hadi dakika 90 za mchezo huo mashabiki wa Madrid
wanaamini kubaki na point moja na kuendelea kuongoza juu kwa point 3 zaidi,
Lion Mess anapachika bao la 3 likiwa la pili kwake katika mchezo huo.
No comments