MIAKA 43 NA SIKU 5 UNITED YAFUFUKA TAFF MORE.
Na John Richard
USISHANGAE
hii ni kawaida kwa Manchester United kuvunja rekodi, na kuandika rekodi,
naimani utakubaliana na mimi ukimkumbuka Sir Alex, alifanya mengi sana na
kuandika historia nyingi sana, Jose Mourinho anakuja United anaandika historia
ya kufunga bao kunako uwanja wa Taff More, nyumbani kwa Burnely.
Antonio Martial aliyeiandikia united bao la kwanza
kunako dakika 21, baaada kuanzisha kaunta ataki na ander herera kumpasia
Martial na kupachika bao la kwanza kwa United, alikuwa tena Martial aliyepiga
pasi ya mwisho kwa Wayne Rooney na kupachika bao la pili kunako dakika 39, hadi
mapumziko Burnely 0-2 Manchester United.
Haikuwa historia tu kwa United kufunga bao kwenye
uwanja wa Taff More, baada ya miaka 43 na siku 5, Antonio Martial anaandika
historia kwenye mchezo huo kwa kufunga bao lake la kwanza na pasi ya bao nje ya
uwanja wa Old Trafford, kunako ligi kuu ya Uingereza toka atue Uingerza
kuichezea United.
No comments