CHIRWA AITAKATISHA YANGA TAIFA
Na John Richard
Mshambuliaji wa klabu ya yanga obrey chirwa
ameongeza matumaini ya kutetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwenye klabu
yake baada ya kuifungia bao la ushindi katika mchezo uliopigwa jana kunako
uwanja wa taifa jijini dare s salaam.
Haikuwa rahisi kwa wana wa jangwani kuibuka na
ushindi katika mchezo huo, ambao walionekana kuzidiwa kimbinu na wapinzani wao
Azam Fc,
Timu zote zilicheza kwa umakini mkubwa huku azam
walionekana kuutawala mchezo takribani dakika 70, na kutengeneza nafasi nyingi
ambazo washambuluiaji wake hawakuweza kuzitumia vyema
Kunako dakika ya 70, Obrey Chirwa aliweza kuwatoka
mabeki wa Azam nq kuweza kupachika bao ambalo liliifanya yanga kuondoka na
ushindi katika mchezo huo na alama tatu muhimu, ambazo zinaifanya yanga kukaa
kilelelni kwa muda wa masaa 24 kabla vinala wa ligi hiyo Simba kushuka uwanjani
masaa machache yajayo kunako dimba la kaitaba kuivaa kagera sugar.
No comments