YANGA YAIPANDIA SIMBA KILELENI
Na John Richard
LIGI kuu Tanzania bara (VPL) imeendelea hapo jana na
kushuhudia mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam, na Yanga kuibuka na alama tatu
muhimu, mchezo uliopigwa uwanja wa taifa jijini dar es salaam.
Haikuwa rahisi kwa Yanga kuibuka na ushindi katika
mchezo huo, kwani Azam walionekana kuutawala mchezo takribani dakika 70, licha
ya kupoteza nafasi nyingi za wazi.
Alikuwa Obrey chirwa alipotumia vyema makosa ya
mabeki wa Azam kwa kushindwa kuwa na
mawasiliano mazuri na kipa wao, baada ya kupoteza mpira na kumkuta Chirwa
kunako dakika ya 70 na kupachika bao lililodumu hadi dakika 90 za mchezo
kumalizika.
Yanga waliingia kwenya mchezo huo wakiwa na kumbukumbu
ya kipigo cha bao 4-0, walichokipata walipokutana na Azam kwenye kombe la
Mapinduzi mwezi January mwaka huu huko Zanzibar.
No comments