WANAFUNZI TSJ, WAASWANIDHAMU, JUHUDI NA UBUNIFU KWANZA
Na John Richard
MKURUGENZI
wa uzalishaji vipindi wa Tabibu Tv, Richard Magambo amewaasa wanafunzi wa fani
ya habari kuwa na nidhamu, juhudi, maarifa na ubunifu ili kuweza kuyafikia
mafanikio, ameyasema hayo ijumaa ya juma lililopita katika sherehe ya Bash,.
Bash
hiyo ilifanyika katika viwanja vya Water World, kunduchi jijini Dar es Salaam,
ikiratibiwa na serikali ya wanafunzi ya chuo cha uandishi wa habari Tsj
kilichopo mitaa ya gereji Ilala Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo alisema.
“Media
sio sehemu rahisi nisehemu yenye changamoto....sio lelemama, inahitaji kujituma,
ubunifu, juhudi, maarifa, nidhamu na uvumilivu wa hali ya juu, Huwezi kufika
bila hivyo vitu, utakata tama tu! kwani, hii fani inachangamoto nyingi sana
katika kutekeleza majukumu yake”.
Magambo
aliyasema hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tabibu Media Group, Benson
Maheya ambaye alitakiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo za Tsj, Bash 2017,
ikiwa ni kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa ngazi ya astashahada na
stashahada na kuwaaaga wale ambao wanamaliza muda wao wa masomo May mwaka huu.
No comments