Header Ads 728*90

YUKO WAPI ROMA


 Na John Richard
HAKIKA siwezi kukaa kimya maaana naona ukimya unaniumiza ndani ya moyo wangu, Sijui nianzie wapi maana wengi wameongea mengi, lakinki nafsi yangu haipati majipu sahihi yakunifanya nilidhike na hii hali.
Na maswali mengi najiuliza nashindwa kujua kuwa akili yangu iko timamau kuwa niko Tanzania? Nchi yenye amani, kama wanavoimba wanasiasa na Watanzania wenye Utimamu wa akili walizo pewa na Mwenyezi Mungu?!.
ROMA, Msanii ambaye anaeleweka kwa kazi zake makini kwa Watanzania Wenye utimamu wa akili na wenye kuiwazia nchi yetu mema, Mwanajeshi anayepamabana kwa niaba ya wanyonge, maskini, wenye nacho na wasio nacho leo hii mnatuambia kuwa AMETEKWA.....!!!!! Tuache kutanianaa maana huu utani naona umevuka mipaka.
Kama kijana naona sasa INATOSHA, Kutazama matendo ya Kipumbavu, kijinga, kishetani na kijesusi yakitokea katika ardhi ya Tanzania hii nikumaanisha kuwa kuna sehemu mambo yamelega lega, ndiyo maana tunafika huko.
ACHA NIVUMILIE HAYA MAZITO LAKINI VIJANA WAKITANZANIA TUTAMBUE KUWA HII NCHI NI YETU NA SISI NDIO MANAHODHA WA KUIKABIDHI KWA WANETU NA WAJUKUU IKIWA SALAMA SALMINI.
NADHANI SI WAKATI TENA WA KUOGOPA LOLOTE IKIWA KUNA DALILI ZOZOTE ZINAZOENDA KINYUME NA UTAMADUNI WA KITANZANIA...
VYOMBO VYA USALAMA TUNAOMBA MTUSAIDIE KUHAKIKISHA USALAMA WA NCHI YETU UNAKUWA IMARA ZAIDI YA NAFSI ZENU, NA MTAMBUE MAJUKUMU YENU NA VIAPO VYENU, MUACHE KUTUMIKA KISIASA, TUMIKENI KITANZANIA 100%.
FREE ROMA, FREE MY NINJA....#VIVA ROMA VIVA

No comments

Powered by Blogger.