SIMBA WANNE WATOROKA MBUGANI
Walinzi wa mbuga
nchini Afrika Kusini wanawatafuta simba wanne waliotoroka kutoka mbuga ya
kitaifa.
Simba hao walitoroka
kutoka mbuga ya Kruger siku ya Jumapili na mara ya mwisho walionekana katika
kijiji cha Matsulu.
Usimamizi wa mbuga
hiyo sasa umewataka wenyeji kuchukua tahadhari
Haijabainika vile
simba hao walifanikiwa kutoroka kutoka mbuga hiyo inayozungukwa na ua.
Mbuga ya kitaifa ya
Kruger ni moja ya mbuga kubwa zaidi barani Afrika ikiwa na ukubwa wa kilomita
19.485 mraba.
Kisa hiki kinatokea
baada ya simba wengine watano kutoroka mbuga hiyo mwezi Mei. Wanne walipatikana
lakini mmoja bado hajulikani aliko.
No comments