CHINA YAZINDUA MELI YA KUBEBA NDEGE ZA KIVITA
CHINA imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.
Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.
Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.
Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.
Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.
No comments