Header Ads 728*90

MIAKA 53 YA MUUNGANO BADO HALI TETE.


Na John Richard
TANGANYIKA na Zanzibar ziliungano mnamo mwaka 1964 mwezi wa 04/26, baaada ya waasisi wa mataifa haya mawili kukubaliana yaaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Amani Karume na ktiana saini kwa udongo wa wa ardhi ya watu wa Zanziba na watu wa Tanganyika kuchanganywa.
Hakika zilikuwa ni busara za hali ya juu sana kwa hawa viongozi kukubaliana na kuwa na mtazamo wa umoja ni nguvu na ni uimara wa kusonga mbele.



Zanzibar inakubali kuungana na Tanganyika ikiwa ni miezi mitatu kufanya mapinduzi na kuwa huru kutoka mikononi mwa mwarabu.

Yapo mengi na sababu nyingi ambazo ziliwafanya viongozi hawa kupata ujasiri wa kuunganisha nchi hizi mbili, na naimani ni mitazamo ambayo ilikuwa chanya kwa pande zote mbili. Ndomana walianza na ushirikiano na sio migogoro.

Leo Taifa la Tanzania linasherehekea miaka 53 ya Muungano, je ni mangapi tunayoyaenzi kutoka kwa waasisi hawa wawili, Mzee Karume na Mzee Nyerere?

Ni changamoto ngapi tumeziibua kutokana na uelewa wetu wa kileo, fikra na tama zetu na sio maslahi mapana ya Watanzania kama walivyowaza waasisi wetu?

Ni kwa kiasi gani viongozi tulionao wanazienzi fikra za Baba wa Taifa na Mzee Karume kwa kuwa viongozi bora kama enzi zao kwa kuwa wakweli na kuwa watawala wa kuyaishi maadili ya uongzi?

Vijana tunathamini vipi Muungano huu kama urithi tulio achiwa na Babu zetu Mzee Karume na Mwalimu Nyerere, kwa kuendeleza na kutafuta njia sahihi ya kuboresha zile changamoto zinazo ibuka kila leo kutokana Uelewa wa Watanzania kupanuka na mabadiliko ya kiteknolojia na ukoloni mamboleo?


Kama Taifa ni wapi tumetoka,  ni wapi tulipo, na ni wapi tunakwenda, Je? Tutafika salama, hili ni swali ambalo kila mtanzania anapaswa kujiuliza kila iitwapo leo na ni njia zipi tuzitumie kuimarisha Muungano huu ili uweze kuwa tunu ya Taifa kwa vizazi na vizazi vya Watanzania wajao?


No comments

Powered by Blogger.