Header Ads 728*90

JE, BARCA ATAWEZA TENA?!!

Paulo dybala aliyeiteketeza barca.
Na John Marwa
BAADA ya kuandika historia ya kupindua matokeo ya kipigo cha bao 4-0 dhidi ya PSG ya Ufaransa, sasa kibarua kingine tena kwa Vibibi vizee vya Torino Juventers baada ya hapo jana kukubali kipigo cha bao 3-0.
Barcelona iliweza kugeuza matokeo dhidi ya klabu ya Paris Saint German (PSJ) kwa kuifunga bao 6-1 katika mchezo wa marejeano wiki chache zilizopita katika hatua ya 16 bora kalbu bingwa ulaya na matokeo kusomeka 6-5.

Ushindi huo uliifanya barcelona kuingia hatua ya Robo fainali na kupagwa dhidi ya Juventers na mchezo wa mkondo wa kwanza ulipigwa hapo jana huko Italia na Barca kupokea kipigo cha bao 3-0.

No comments

Powered by Blogger.