MC' PILIPILI ATOANSOMO KWA VIJANA WENYE VIPAJI
Na John
Richard
JINA la Emmanuel Mathias MC’ Pilpili’ hakika limezidi kuwa Lulu katika sherehe
mbalimbali katika jamii ya kitanzania, hii ni kutokana na kipaji chake cha
ushereheshaji alichojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Kupitia
kipaji chake cha ushereheshaji MC’ Pilipili amejizolea umaruufu mkumbwa
miongoni mwa watanzania walio wengi na kufanya thamani ya kazi yake kuwa juu
kila uchao.
MC’
Pilipili kupitia uchekeshaji na ushereheshaji ameweza kuvuka mipaka ya Tanzania
kwa kwenda Kenya, Uganda, Rwanda pamoja na Afrika ya kusini safari ambazo
zimemfanaya ajitangaze zaidi na kufahamika nje ya mipaka ya Tanzania.
Akizungumza
na Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (TSJ), katika sherehe ya Bash
iliyofanyika tarehe 7, mwezi huu, katika viwanja vya Water World, Kunduchi
Jijini Dar es Salaam, MC’ Pilipili alisema alipenda kuwa mwandishi wa habari
angali yupo shule ya msingi lakini Mama yake alikuwa kikwazo.
“Nilipata wakati mgumu sana kufanya uamuzi kwani nilipenda kuwa Mwandishi wa habari na wakati
huo huo mama yangu alisisitiza niende ualimu kwani hata katika familia yetu
hakuna hata mmoja aliyewahi kuwa mwandishi wa habari,”.Alisema MC’
Hakika
uwepo wake katika Bash hiyo uliwafanya wote waliohudhuria kuona hawakukosea
kujumuika katika tukio hilo la Bash ambalo huandaliwa na Serikali ya Wanafunzi
Chuoni hapo kila mwaka.
Licha
ya kunogesha sherehe hiyo alitoa Sh, Laki mbili za Kitanzania kwa kuinunua Keki
iliyoandaliwa na Serikali ya Wanafunzi (TISJOSO), sambamba na kiasi hicho cha
fedha alichokitoa, pia aliahidi kununua kompyuta moja kwa ajili ya Chuo.
MC’Pilipili
akiwaasa wanafunzi wa TSJ, na vijana wa kitanzania kutumia vipaji vyao na sio
kulazimisha vitu ambavyo ni vigumu kama vile kusoma, Alisema..
“Kipaji
kinaweza kukupeleka mbele yawakuu” akitolea mfano wa watu wa kwenye Biblia kama
Mfalme Daudi na Yusuph ambao walitumia vipaji vyao na wakainuliwa na Mungu.
“Napenda
kutumia usemi unaosema ‘Sherehe ni Mc”. Aliyasema hayo akiwashauri
washereheshaji wenzake kufanya kazi hiyo kwa kuhakikisha wanasoma vitabu,
kuangalia intenet kuona nini wanatakiwa kufanya ili wafanye kazi hiyo katika kiwango
kizuri.
Pia anaishauri serikali kurudisha masomo ya
sanaa na kuweka walimu maalum wanaojua sanaa kwa
viwango na ubora unaoendana na ulimwengu wa teknolojia tuliyopo sasa.
No comments